Skip to content
edutymes
Menu
  • Home
  • Updates
  • Scholarships
  • Study Notes
  • Results
  • Past Papers
Menu

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili NHIF

Posted on January 17, 2023 by Edutymes


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya “National Health Insuarance Fund” (NHIF) inapenda kuwa taarifu watanzania wote walioomba kazi zilizokuwa zimetangazwa kwa niaba ya Mfuko huo kuwa, inatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji wote watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili huo wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama ilivyoanishwa katika jedwali hapo chini katika kila nafasi husika.
  1. Kila Msailiwa atapaswa kufika na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi vitambulisho vinavyotambulika ni pamoja na Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Hati ya kusafiria, na Kitambulisho cha Uraia.
  1. Kila Msailiwa atapaswa kufika na Vyeti Halisi (Original Certificates) vya kuanzia kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  1. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  1. Sekretarieti ya Ajira haitahusika na gharama zozote zitakazotumiwa na wasailiwa katika kufanikisha kuhudhuria usaili huo.
  1. Kila Msailiwa atapaswa kuzingatia tarehe na eneo alilopangiwa kufanya usaili.
  1. Kila Msailiwa atapaswa kufika na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
  1. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA) na watapaswa kufika na vielelezo hivyo.
  1. Waombaji wote wa nafasi zilizotangazwa kwa niaba ya Mfuko huo ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Download orodha. May 5, 2017 (TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI-MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF))

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts

  • Check JCE Results 2023/2024 Online Now! – Botswana
  • Botswana JCE Results 2023/2024: Check SMS/Online
  • Botswana PSLE results 2023/24 – here’s direct link to check
  • My Results Botswana BEC: JCE & PSLE results 2023
  • MANEB JCE Results 2023 – JCE Pass List

Recent Comments

  1. Owami Watts on Limkokwing University Swaziland Application form 2023/2024

Categories

  • All Posts
  • Home
  • About us
  • Privacy Policy
  • Contact us
©2026 Edutymes | Design: Newspaperly WordPress Theme